Josho La Mifugo
Kijiji cha Kinyangiri kilichopo wilayani Mkalama takribani kilimita 20 toka mji wa Iguguno kina idadi kubwa ya mifugo ikiwemo ng'ombe na mbuzi. Idadi kubwa ya mifugo hii inatokana na mazingira rafiki ya mifugo kama vile hali ya hewa, aina ya uoto unaopatikana pamoja na ukubwa wa ardhi ya malisho. Hivyo basi, mifugo ni moja ya shughuli za kitega uchumi na maendeleo kijijini hapo.
Uwingi wa mifugo hii umepelekea kuwa na uimarisho katika afya na tiba ili kuboresha afya za mifugo. Hivyo basi, katika kijiji cha Kinyangiri kumejengwa josho kwa ajili ya mifugo hii. Josho ni sehemu maalumu ambapo wanyama huweza kaguliwa na kupewa tiba pamoja na chanjo.
Picha hizi chini zinaonesha sehemu mbali mbali za josho ambapo ndipo mifugo hudumbukia kwenye maji yenye dawa na sumu ya vijidudu. Josho kwa kawaida ina sehemu kuu tatu. Kwanza, wanyama hukusanywa na kuingia katika mlango mkuu, hapa huwa ni kupana na kupo usawa wa ardhi.
Baada ya sehemu ya kwanza, mifungo kisha huelekea sehemu ya pili ya josho ambapo hupita mmoja mmoja kwenye njia nyembaba iliyo maalumu kwa mnyama mmoja tu kupenya. Mfugo hufuata hiyo njia fupi na kisha kudumbukia kwenye shimo lililojaa maji ambalo ni sehemu ya pili.
Makala na picha zote na Ahmed Shams
Asante kwa makala nzuri.
ReplyDelete